Featured

Soma vitabu Tanzania

SOMA VITABU TANZANIA📚:
Kama una tabia hizi 10, huwezi kamwe kufanikiwa kwenye maisha.

Rafiki yangu mpendwa,
Sipendi kuwa mtu wa kuleta habari mbaya kwako, lakini ukweli huwa haujali.
Ukweli huwa unabaki kuwa ukweli iwe unapendwa au haupendwi.

Hivyo badala ya kutumia mbinu ya mbuni, kuficha kichwa kwenye mchanga ili kutokuiona hatari, ni vyema tukaiona hatari na kuchukua hatua sahihi.

Kuna watu huwa wanasema mafanikio hayana fomula. Watu hao huwa hawajui. Kuna vitu ambavyo waliofanikiwa wote wanavyo na kuna vitu ambavyo walioshindwa wanavyo.
Hilo haliwezi kuwa bahati, kuna kanuni inahusika.

Mafanikio ni kama sayansi, yana kanuni ambayo ikifuatwa basi mtu anapata matokeo mazuri bila kujali yuko wapi au tuko kwenye hali gani.
Sheria ya mvutano ya dunia inafanya kazi Tanzania kama inavyofanya marekani. Na hivyo pia ndivyo mafanikio yalivyo, kuna vitu ukivifanya utafanikiwa, iwe upo Tanzania au Marekani. Na kuna vitu ukivifanya utashindwa.

Tumeshajifunza sana vile ambavyo ukifanya utafanikiwa. Leo ni siku ya kujifunza vile ambavyo ukifanya utashindwa ili uweze kuviepuka kama unataka mafanikio kwenye maisha yako.

Kuna tabia kumi ambazo ni sumu sana na zipo kwa wengi walioshindwa. Ukizijua hizi na kuzikana kwenye maisha yako, utaweza kufika kwenye mafanikio makubwa.
Karibu ujifunze tabia hizo kumi.

 1. Kutokujitambua.

Kama hujijui wewe ni nani na kwa nini uko hapa duniani, utatumia muda wako mwingi kuhangaika na kila kinachokuja mbele yako.
Kama hujui kusudi la maisha yako na huna ndoto kubwa unazopambana kufikia, utaridhika na chochote kinachokupa chakula na malazi.
Tofauti kubwa ya waliofanikiwa na walioshindwa ni kujitambua.
Tatizo la kujitambua ni kwamba hakuna anayeweza kukufanyia, ni kitu unapaswa kufanya mwenyewe.
Hivyo kama mpaka sasa hujajua wewe ni nani (siyo jina lako wala cheo chako) na uko hapa duniani kwa sababu gani, basi hilo linapaswa kuwa jukumu lako la kwanza.
Wanasema kusudi la maisha ni kuishi maisha yenye kusudi.
Huwezi kufika kwenye mafanikio makubwa kama hujajitambua mwenyewe. Hata ukikutana na bahati nzuri, kama hujajitambua utaishia kuipoteza.
Jitambue na yaishi maisha yako, hiyo ndiyo njia ya kufikia mafanikio makubwa.

 1. Kutokujisomea.

Kujisomea vitabu na kujifunza vitu vipya ndiyo nguvu ya kuleta miujiza mikubwa kwenye maisha yako.
Chochote unachotaka kujua kipo kwenye vitabu.
Changamoto na magumu unayopitia kuna wengine walishayapitia na uzuri ni waliyaandika kwenye vitabu, wajibu wako ni kusoma uzoefu wao na kuchukua hatua kwa hali yako.
Waliofanikiwa ni wasomaji wazuri, wanajua kuna mengi hawajui.
Walioshindwa siyo wasomaji wa vitabu, wanajiambia tayari wanajua kila kitu au hawana muda wa kusoma.
Ni sawa na kukutana na mtu ambaye amekula chakula mara moja na kusema ameshiba milele, hakuna kitu cha aina hiyo, utaendelea kula mpaka siku ya kufa.
Kadhalika unapaswa kuendelea kujifunza kila siku mpaka siku unakufa.
Kama hupendi kujisomea, hakuna namna utafanikiwa.

 1. Kutokuweka akiba.

Kama unatumia kipato chote unachoingiza, hakuna namna unaweza kufanikiwa. Haijalishi kipato ni kidogo au kikubwa kiasi gani.
Hebu fikiria mkulima ambaye anakula mavuno yake yote bila kuacha mbegu, hawezi kufanikiwa kwenye kilimo.
Mafanikio yako hasa kwa upande wa fedha hayatokani na kiasi unacholipwa, bali jinsi unavyotumia kiasi hicho.
Kuweka akiba ni tabia unayopaswa kuijenga, hakutegemei kiasi cha kipato unachoingiza.
Usiseme huweki akiba kwa sababu kipato ni kidogo, kama huwezi kuweka akiba kwenye kipato kidogo, hutaweza kuweka akiba kipato kikiwa kikubwa.
Jijengee tabia ya kuweka akiba kwenye kila kipato chako na kisha kuwekeza ili izalishe zaidi. Hiyo ndiyo mbegu ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.

 1. Kutokujiamini.

Kama hujiamini wewe mwenyewe, hakuna mwingine anayeweza kukuamini. Na kama hakuna anayeweza kukuamini, huwezi kufanikiwa.

Maana chochote unachotaka ni wengine wanacho na watakupa pale wanapokuamini.
Waliofanikiwa wanajiamini mno, wanajiamini kupitiliza. Wakati mwingine wanaigiza kujiamini mpaka wanajiamini kweli.
Angalia timu mbili zinazokwenda kwenye mashindano yoyote, japo kuna moja itashindwa, lakini zote zinaingia uwanjani ziliwa zinajiamini kwa asilimia 100 na bila ya shaka yoyote kwamba zinakwenda kushinda.
Na hata tafiti zinaonesha ushindi huwa unapatikana kabla hata timu haijaingia uwanjani, kutokana na kiwango cha kujiamini.
Kama hujiamini, umeshashindwa kabla hata hujaingia kwenye mapambano.
Jiamini sana, jiamini mpaka wengine waone kama umechanganyikiwa na watakapoona imani yako kwako na kwa mafanikio yako haitikisiki, watakuamini na kuwa tayari kushirikiana na wewe.
Ukijitambua na kujiamini bila ya kuwa na shaka, hakuna kinachoweza kuwa kikwazo kwako.

 1. Kulaumu na kulalamika.

Kuwalaumu na kuwalalamikia watu wengine ni kukubali kuyaweka maisha yako kwenye mikono yao na waamue kuyafanya watakavyo.
Huwezi kufanikiwa kama hujashika hatamu ya maisha yako, kama hunayafanya maisha yako kuwa wajibu namba moja kwako.
Kwa lolote linalotokea kwenye maisha yako, wewe ndiye unayewajibika kwa asilimia 100. Usilaumu wala kumlalamikia yeyote.
Siyo serikali, siyo wazazi, siyo ndugu, siyo mazingira na wala siyo hali ya uchumi. Ni wewe ndiye unayewajibika na maisha yako, shika hatamu, chukua hatua sahihi ili ufanikiwe.

 1. Kuahirisha mambo.

Unapanga vizuri kitu unachopaswa kufanya, lakini unapofika wakati wa kufanya unaahirisha na kujiambia hujawa tayari, utafanya kesho au wakati mwingine.
Kama unataka kufanikiwa futa kabisa msamiati wa kesho kwenye maisha yako.
Kila unapopanga kitu cha kufanya na wakati wa kufanya ukafika ukajisikia kuahirisha, jiambie nitafanya sasa na kisha anza kufanya.
Huhitaji kufanya kwa kiasi kikubwa sana, wewe anza kufanya na utajikuta unaendelea kufanya.
Nidhamu binafsi ni hitaji muhimu sana kwa mafanikio yako. Kupanga tu haitoshi, lazima utekeleze kama ulivyopanga.
Usiwe mtu wa kuahirisha, kuwa mtu wa kuchukua hatua.

 1. Kutokutoa kafara.

Unataka ufanikiwe halafu hutaki kubadili namna unavyoishi maisha yako. Hiyo ni sawa na kuwa na pipi, unataka kuila lakini pia ubaki nayo.
Hiyo sayansi haipo, kupata bora ambacho huna sasa, lazima upoteze kizuri ulichonacho sasa.
Yote tunayojifunza hapa kuhusu mafanikio, yatafanya kazi kama utakuwa tayari kutoa kafara.
Ili uweze kuweka akiba lazima utoe kafara kifedha, uachane na baadhi ya matumizi mazuri na unayoyapenda ili uweke akiba.
Ili upate muda wa kujisomea, lazima utoe kafara ya muda, uachane na mazuri unayofanya sasa ili upate muda wa kujisomea na kuwa bora zaidi.
Ili uzungukwe na watu sahihi, lazima uwe tayari kuwapoteza wale ulionao sasa.
Kuwa tayari kutoa kafara, kuwa tayari kutengana na unachokipenda sana ili uweze kupata makubwa zaidi.

 1. Kutokuwa king’ang’anizi.
  Safari ya mafanikio siyo ya njia iliyonyooka. Kuna milima na mabonde na pia kuba kona kali.
  Utakutana na vikwazo na changamoto za kila aina. Kama mawazo yako ni mambo kuwa rahisi, hutafika mbali.
  Utashindwa, utaanguka, lakini haimaanishi huo ndiyo mwisho wa safari.
  Unapaswa kung’ang’ana na kuendelea na safari yako bila kujali nini umekutana nacho.
  Ili ufanikiwe, lazima ujipe agano kwamba utapata unachotaka au utakufa ukiwa unakipambania.
  Kama una mbadala wa hilo, kama utakutana na ugumu na kukimbilia kufanya kitu kingine, hutaweza kufanikiwa.
  Utahangaika na mengi lakini yote utakutana na magumu na kukimbia.
  Ng’ang’ana hasa mpaka upate kile unachotaka.
 2. Kuamini njia za mkato.

Kama unaamini siku moja utalala masikini na kuamka tajiri basi jua utakufa masikini.
Kama unasubiri ‘zali la mentali’, kwamba ukutane na bahati ambayo itakutoa ulipo na kukufikisha juu unajidanganya.
Kama unaamini kuna siri ulizofichwa ambazo wachache tu ndiyo wanazijua utabaki kwenye mahangaiko.

Featured

UMUHIMU WA KUSAJILI BIASHARA/KAMPUNI

ZIJUE FAIDA ZA KUISAJILI BIASHARA KUWA KAMPUNI DHIDI YA JINA LA BIASHARA NCHINI TANZANIA

KUTOKA MAGIRA INSPIRE
*Inaandikwa na
GODFANS
Habari Mjasiliamali na mpambanaji, Inawezekana bado unajiuliza na kujishauri kuhusu umiliki wa kampuni au urasimishaji wa biashara zako lakini bado hujafikia muafaka, na pengine hujawahi hata kufikiria kabisa na hapa huenda ikawa ni mara yako ya kwanza kufahamu kuhusu makampuni, hali hiyo hupelekewa na sababu mbalimbali ikiwemo kutokujua kabisa, yaani mtu mwingine akisikia neno ‘Kampuni’ tayari yanamuijia kichwani kwake majengo makubwa, magari, wafanyakazi wengi watanashati, akaunti ya fedha benki yenye pesa nyingi, n.k. hivyo mtu huyo hujiona yeye sio hata wa kulitaja neno kampuni.
Pia sababu nyingine kutokuelewa ni namna gani biashara zake zinaweza kusajiliwa na kuendeshwa kama kampuni, na zaidi ni kutokuelewa umuhimu wa kuwa na kampuni, yaani unakuta mtu anafanya biashara nyingi na kubwa mfano kusafirisha mbao kutoka mkoa wa Iringa kuleta Jijini Dar es Salaam, au kutoa samaki Mwanza kuleta Dar es Salaam, au biashara ya kukopesha pesa, n.k. lakini anaona biashara zinakwenda vizuri tu na hivyo asione hata umuhimu wa kuzirasimisha biashara zake.

Unapoamua kufanya biashara ni vema kuzingatia mfumo wa usajili wa biashara yako na kuamua vema ili kufanya biashara katika mazingira mazuri hususani ya kisheria, ndiyo sababu MAGIRA INSPIRE huwa tunawashauri kwa weledi wale wanaosajili biashara zao ili wafanye maamuzi sahihi. Kwa kifupi, unaweza kusajili Jina la biashara, mfano ‘Ifakara intersperses’, endapo nikiwa nafanya biashara ya kusafirisha mizigo, au ‘Ifakara Microcredit’ endapo ninafanya biashara ya kukopesha pesa, na nitaruhusiwa kuendesha shughuli za biashara (Business activities) kuanzia moja mpaka Nne tu, endapo nimesajili Jina la biashara.biashara

Lakini leo nitajikita katika Kampuni, na mada ya Kampuni ni kubwa mno, ila nitakufafanulia faida chache muhimu za kuisajili biashara yako kama kampuni, kwani wengi huuliza, “kuna faida gani za kuwa na kampuni?”
kama nilivyotangulia kusema hapo juu kuwa jina la biashara linakupa ruhusa ya kufanya shughuli za biashara zisizozidi nne, tofauti na kampuni ambapo unaweza kuorodhesha shughuli za biashara mpaka 50, yaani hata zile ambazo unatarajia kuzifanya kipindi kijacho, zinaweza kutambulika sasa na hapo baadae likabaki suala la upatikanaji wa leseni ya biashara hiyo kwenye halmashauri za manispaa au wizarani pamoja na vibali husika kutoka kwenye mamlaka za serikali, mfano TFDA, TBS na kadhalika.

Moja kwa moja tuangalie umuhimu wa kusajili kampuni, Mara kwa mara huwa napokea simu za wateja wetu wengi sana wengine wannitumia ujumbe, wengine hunicheki whatsapp, wengine kwenye E-mail yangu, maswali wanayoniuliza ni kuhusu faida za kufungua kampuni, huwa nawaeleza kwa ufupi lakini huwa wanaonekana kutaka kufahamu zaidi suala zima la kodi, kwasababu suala hili la kodi limekuwa likiulizwa na wengi sana, pia wafanya biashara wengi wamekuwa wakihitaji kufahamu kuhusu kodi za makampuni, wajasiriamali na wafanya biashara na wengine wengi nimekuwa na majadiliano nao kuhusu suala hili, nitajitahidi kueleza kwa undani na kwa ufupi kama ifuatavyo:
Kodi ya makampuni ni kodi inayotozwa katika mapato yanayotozwa kodi (faida) ya asasi kama vile makampuni yenye dhima ya ukomo. Kampuni yenye dhima ya ukomo (Limited Liability company) inalipa kodi ya shirika (Corporate Tax) ambayo ni 30% kwa viwango vya sasa kutokana na Sheria ya mapato iliyofanyiwa mapitio mwaka 2008 na kodi hii hukokotolewa kwenye faida ya mwaka, hivyo basi, kampuni itakuwa na unafuu mkubwa kwenye kiwango hiki ukilinganisha na endapo biashara hiyo ingekuwa ina umiliki binafsi(Jina la biashara), hasa hasa pale ambapo kampuni inazidi kukua na kuongeza shughuli za biashara.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), mapato yanayotozwa kodi (faida) katika kodi ya makampuni yanahusisha:

 1. Faida inayotokana na shughuli za biashara,
 2. Faida inayotokana na uwekezaji (isipokuwa migawanyo ya faida ambayo imetozwa kodi tofauti kama kodi ya mwisho),
 3. Kodi inayotokana na mapato ya makampuni yenye hasara za muda mrefu ambazo hazijasamehewa kwa miaka mitatu mfululizo.

Mpenzi msomaji wa makala hii, fahamu kwamba zipo faida nyingi zitokanazo na uendeshaji biashara kama kampuni, kwani makampuni hunufaika na misamaha ya kodi pamoja na mapunguzo ya kodi kutokana na aina ya shughuli mbalimbali ambazo inajihusisha nazo.
Kwa mfano, kwa mujibu wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Kampuni mpya iliyoanzishwa na ambayo inajihusisha na utengenezaji wa madawa ya binadamu na bidhaa za ngozi na ina mkataba wa makubaliano na Serikali ya Jamhuli ya Muungano wa Tanzania itatozwa kodi kwa kiwango cha 20% kwa kipindi cha miaka mitano mfulizo kutoka mwaka walipoanza uzalishaji, hii ni pungufu ya 10%, pia kama kampuni haijapata faida, itaandaa vitabu vyake vya mahesabu na kuviwasilisha kwenye mamlaka ya mapato na haitalipa chochote, kodi itatozwa kwenye faida kama ilivyoainishwa kwenye sheria na si vinginevyo, tofauti na biashara binafsi(sole proprietors).

Watu binafsi (sole proprietors) hukadiriwa kodi kutokana na mauzo yao, kwa mfano;
Kwa mtanzania (bara) kodi kwa mtu binafsi endapo mapato yake yanazidi Shs 720,000/= kiwango cha kodi anayotozwa ni Shs 98,100/= jumlisha na 30% ya mapato yanayozidi Shs 720,000/=, lakini kwa kampuni, huenda mapato yakawa ni hiyo hiyo Shs 720,000/= kwa mwezi, na gharama na matumizi vikawa ni Shs 300,000/=, kwa hiyo faida ni Shs 420,000/=, kwa hiyo kwa mwezi huo kwa kampuni kodi itakokotolewa kwa kupata 30% ya faida, yaani Shs 420,000/= ambayo ni Shs 126,000/=, tofauti na mtu binafsi ambaye atalipa Shs 98,100/= jumlisha 30% ya mapato yanayozidi 720,000/=, tuseme ni Shs 800,000/= ambayo ni Shs 240,000/=, hivyo kutakiwa kulipa kiasi cha Shs 338,100/=. japo kwa mwaka mapato yasiyozidi Shs 2,040,000/= kwa watu binafsi hayatozwi kodi, lakini kwa hali ya kawaida ya biashara na bei ya vitu na huduma kuwa juu, ni rahisi kwa mapato kuzidi kiwango hicho pamoja na kupata faida kidogo, lakini kwa kuwa ni mtu binafsi mzigo wa kodi ukakuelemea vile vile.
Kwa hiyo, hapa tunaona unafuu wa kusajili kampuni, na ndivyo ambavyo Shinebright Consulting tunawashauri wawekezaji, na ukihitaji kufahamu zaidi wasiliana nasi au tutembelee ofisini.

Pia, Unapoisajili biashara yako kuwa kampuni unapunguza hatari ya kuwepo kwa mvutano wa kimaslahi baina ya waanzilishi, kwani wamiliki wa kampuni maslahi yao kwenye kampuni husika ambayo wanaimiliki yanakoma kulingana na idadi ya hisa wanazozimiliki, au kiwango cha uwekezaji kutokana na hisa walizozinunua, na si vinginevyo. Tumezoea kuwepo na makubaliano holela ya mdomo au maandishi kwamba mtu A na mtu B wamekubaliana watafanya biashara fulani kisha watagawana faida, halafu baadae wanaanza kuingia kwenye migogoro kwamba huyu anasema biashara ni ya kwake na yule anasema ni ya kwake, au katika kugawana faida kila mmoja anaweza kumzidi mwenzake na hupelekea watu kugombana hata kusababisha hasara kubwa, lakini kama watu wameamua kufanya biashara kwa kuisajili kwanza kuwa kampuni, biashara hiyo inakuwa na utaratibu rasmi wa kisheria katika kuisimamia na anapotaka kujiondoa mmoja wapo, unafuatwa utaratibu rasmi ambao upo kwa mujibu wa sheria, na si vinginevyo.
Hivyo basi, kusajili kampuni kunaondoa migogoro mingi ambayo inaweza kujitokeza baadae, hasa biashara inapokua kubwa sana au inapoonekana kukwama kukua.

Hali kadhalika kusajili kampuni kunapelekea kuwepo na mazingira rafiki ya kukuza mtaji. Kuongeza mtaji wa kampuni kunaweza kusaidia katika upanuzi wa biashara au kupelekea ukuaji. Taratibu za kitaalamu na kisheria zimeainisha namna nzuri za kuongeza mtaji aidha kwa kuuza hisa zilizobakia kwenye kampuni kwa wamiliki waliopo ili kuongeza mtaji, au kwa kuongeza wanahisa wapya na kununua hisa za kampuni ili kuongeza mtaji, na pia ni rahisi hata kuwakaribisha wawekezaji wengine ndani au nje ya nchi wakanunua hisa na kuongeza mtaji bila kuathiri shughuli za kampuni.
Sio rahisi kama mtu unafanya biashara ambayo haijasajiliwa kuwa kampuni, kuwakaribisha watu wengine kuwekeza pesa zao kwako, usalama wa kuwekeza pesa ni pale ambapo biashara imesajiliwa kama kampuni, kwani hata katika macho ya kisheria kampuni inatazamwa kama taasisi nyingine tofauti na wamiliki wa kampuni hiyo (separate entity).

Jambo lingine muhimu kabisa ni kuwepo kwa ukomo wa dhima binafsi (Limited liability).
Kampuni mbele ya macho ya sheria ni taasisi inayosimama yenyewe tofauti na wamiliki wa kampuni hiyo (separate legal entity), na kampuni inaweza kushitaki au kushitakiwa mahakamani (veil of incorporation), hivyo basi, endapo biashara inapata misukosuko katika uendeshaji, umiliki au uwekezaji, n.k. inaweza kuwajibika yenyewe na wamiliki wa kampuni hiyo wasipoteze kitu chochote isipokuwa tu uwekezaji wao kwenye kampuni hiyo. Mfano; katika biashara, mmekopa pesa benki au kwenye taasisi yoyote ya fedha na biashara ikashindwa kufikia malengo ikajikuta inaingia kwenye madeni makubwa, ni kampuni ndiyo itakayowajibika kwenye madeni hayo, na wamiliki wa kampuni watakachopoteza ni uwekezaji wao kwenye kampuni husika. Pia endapo bidhaa au huduma zilizotolewa zimeisababishia hasara kampuni, itakayowajibika ni kampuni yenyewe. Hii ni tofauti na biashara binafsi (Sole proprietorship) ambapo mmiliki wa biashara anawajibika moja kwa moja yeye mwenyewe kwasababu kisheria ni yeye mwenyewe ndiye anayetambuliwa na si vinginevyo.

Mwisho tuangazie suala muhimu sana nalo ni kujitambulisha na kujitengenezea hadhi kibiashara, jambo ambalo linaweza kuboresha mahusiano mazuri baina ya kampuni yako na wateja (Branding). Leo tunaona makampuni makubwa kama Vodacom, IPP Media, Mbeya Cement, CRDB n.k. namna yalivyojitengenezea namna ya kutambulika kwa wateja wao, unapolisikia tu jina la kampuni mojawapo limetajwa unapata picha halisi na kubwa juu ya biashara ya kampuni hiyo kwa uharaka. Kuendesha biashara iliyosajiliwa kama kampuni pia kunakupelekea kuaminika na ni rahisi hata kuingia mikataba mikubwa aidha na makampuni mengine au na serikali. Kwa mfano, serikali inatangaza zabuni ya ujenzi wa barabara na mradi huo gharama yake ni Shs 30,000,000/=, pesa hizo zote sio rahisi kuingia mkataba na mtu binafsi au watu wachache binafsi wasio rasmi kisheria, lakini ni rahisi kuingia mkataba na kampuni, na pia hata kukopeshwa kwenye mabenki na makampuni ya fedha mikopo mikubwa ya biashara ni rahisi endapo mmesajiliwa kama kampuni kuliko binafsi (individuals).

Leo DILEX BUSINESS SOLUTION imekuwa na nafasi kubwa ya kuhudhuria mikutano mikubwa na kukutana na wawekezaji wa nje wengi na wa ndani wengi ambao wanamtazamo mpana kibiashara na tumekuwa tukiwashauri wawekezaji wa ndani na nje ya nchi namna ambavyo wanaweza kunufaika endapo watasajili biashara zao kuwa kampuni na sio kuziendesha kiholela au kienyeji.
Jambo moja ambalo nilitaka kulisahau, unaposajili kampuni inakurahisishia wewe hata namna ya kuirithisha biashara, kwa mfano; Baba na mama mmesajili kampuni na mtoto wenu amefikisha umri wa miaka 18, mnaweza kumuongeza kama mwenye hisa (Shareholder) na biashara zikaendelea kama kawaida, wakati anaendelea kupata elimu, anakuwa anafahamu fika kwamba anasoma ili asimamie biashara ambayo yeye mwenyewe ni mmiliki halali wa sehemu ya biashara hiyo kutokana na kiwango cha hisa anazozimiliki, hivyo kumfanya asome kwa bidii bila kuwa na hofu juu ya soko gumu la ajira.

Zipo faida nyingi na muhimu sana za kusajili biashara yako kuwa kampuni, usichelewe kwani wakati ni sasa, rafiki yangu mmoja nilimsikia akisema kuwa “Kusajili kampuni ni lazima uwe na gari kwanza, lazima” aliongea kwa kusisitiza, lakini kwa kumsaidia na kwa faida ya wengi, kusajili kampuni zipo taratibu maalum zilizowekwa na mamlaka husika yaani BRELA (Wakala wa usajili wa makampuni na majina ya biashara), na sisi kama washauri nafasi yetu ni kukushauri uwe na ufahamu juu ya makampuni na uendeshaji wake, umuhimu wa kusajili biashara na kukupa msaada wa kitaalam ili uweze kufanya maamuzi sahihi na yenye tija, ili kutimiza malengo yako kwa wakati na bila gharama zinazoepukika.
mimi ni mr godfans speker, Life coach na mchambuzi wa masuala ya biashara, mjasiriamali mdogo

0769176064

Featured

KWANINI MASKINI WANABAKI HIVYO…

U- K -W -E -L -I

KWANINI MASKINI WANABAKI HIVYO…..

Mtu mmoja aliwahi kusema, “ukichukua fedha zote ulimwenguni na ukizagawa sawa sawa kwa kila mmoja, baada ya mda hela zitawarudia wale walio kuwa nazo mara ya kwanza” Kwanini?

 ......."Maskini ni watumiaji wakati matajiri ni wawekezaji"......

Nioneshe mtu maskini, nitakuonyesha mtu anae pishana na fursa mara kwa mara.

Mtu anaeona changamoto ndani ya kila fursa badala ya kuona fursa ndani ya kila changamoto.

Kuwa MWANAUME sio cheo, ni jukumu. Inamaanisha unapaswa kuwwajibika kiuchumi Asubuhi, Mchana na Usiku.

Lazima uchukue maamuzi magumu ili upate matokeo makubwa.

Unapaswa kupanga na kuweka mikakati, lazima uthamini faida na fedha kidogo unayoipata. Lazima uwe makini na mwenye nia kama unataka kufanikiwa.

Watu wasiofaa kabisa kuhudumiwa hapa duniani ni WATU MASKINI.

UMASIKINI Ni kupishana na fursa kila wakati.

Angalia sababu hizi
1) ukiwapa bure, watahisi ni mtego.

2) ukiwaambia ni mradi mdogo wawekeze, watakwambia hauwezi ukaleta faida

3) ukiwambia waingie kuwekeza katika ukubwa, watakwambia sina hela

4)ukiwaambia wajaribu vitu vipya, watakwambia hamna uzoefu: umewahi kuona wapi hichi kitu kimefanikiwa? Nani amewahi kufaidika nacho?

5) Ukiwaambia ni biashara ya kawaida ya kila siku, watakwambia ni kazi ngumu sana hiyo

6) ukimwambia ni mpango biashara mpya, atakwambia mimi huwa siongeagi sana na watu alafu ni kwa miaka mingapi sasa huu mpango biashara umekuwepo?

7) ukimwambia afungue duka, atakwambia nitakosa uhuru ntashindwa kufanya mambo mengine.

8) ukimwambia afate mpango wa biashara yake kwa mwaka mmoja, atakwambia ni mda mrefu sana huo, siwezi subiri.

9) ukimuuliza ni nini anaweza kufanya, atakwambia “naweza kufanya chochote”

10) wanapenda kuwauliza marafiki zao, ambao ni kama wao juu ya mtazamo wao. Hata maandiko matakatifu yameeleza kuwa vipofu, kamwe hawaongozi vipofu wenzao.

11) wanafikiri zaidi ya mkufunzi wa chuo kikuu na wanafanya kidogo kuliko kipofu.

12)Akienda kanisani anasema hana kabisa sadaka lakini wakati huo huo anatoka na kununua maandalizi (ANAAMUA KU’INVEST CHOONI KULIKO KWENYE UFALME WA MUNGU)

Changamoto kubwa sana watu maskini walio nayo, ni kukosa kuchukua hatua

Wanafurahia kasehemu kasiko na mahangaiko. Wanakwea katika dimbwi la ulimwengu wao na ufahamu wao ….

NB;
kuna hatari katika kuchukua hatua, lakini ni hatari zaidi kutokuchukua hatua..

Bora kuchukua hatua.

With JULIUS Michael (micle darl)

Featured

MAMBO 15 NALIYOJIFUNZA KUTOKA KWENYE KITABU CHA KUTHUBUTU NA AMINA SANGA

.

1.Kiwango chako cha Elimu hakina mahusiano na mafanikiwa yako, bali ujinga unamahusiano ya moja kwa moja na umaskini wako.

2.Usichague kazi ya kufanya. Sio lazima uanze kufanya kazi unayoipenda bali penda kazi unayoifanya na uifanye kwa viwango. mfano mwandishi ktk ukurasa wa 4, Elienda kufanya mafunzo kwa vitendo(field) akawa anauza clips.

3.Huhitaji fedha au mtaji kuanza bali unahitaji wazo(idea).

4.Mwandishi anatufundisha huhitaji kumfurahisha kila mtu juu ya kila kitu unachofanya, Namnukuu…….Walinitania sana lakini mwisho wa siku mi naingiza hela.

5.Badili namna unavyofikiri, namnukuu pia hapa mwandishi. “Anasema…….Binafsi haikunusumbua kwa sababu nafahamu kusoma ni kitu kingine na kuelimika na kitu kingine.”

6.Mwandishi amenifundisha kuwa maarifa ni msingi wa kuthubutu.

7.Mwandishi amesisitiza kulifanyia kazi wazo(idea) ulilonalo kwa maana vyote unavyoviona duniani vimetokana na wazo la mtu lililokuwa kichwani mwake na akaamua kulifanyia kazi kwa bidii.

 1. Mwandishi amesisitiza kuwa lazima mtu makini awe na malengo na ni lazima awajibike ktk kutekeleza malengo yake, usiwe mzungumzaji sana bila kufanyia kazi malengo yako.

9.Mwandishi ametaja kuwa watu ni nguzo muhimu katika kuthubutu, amesisitiza kuwa pamoja na kwamba tunahitaji watu lakini si kila mtu nisahihi kumshirikisha mambo yako muhimu.

10.Mwandishi ametabayanisha kuwa ili kuweza kufanikiwa ktk eneo lako la uthubutu unahitaji kuwa na maarifa sahihi. Ameeleza kuwa si kila aliyeshindwa ktk uthubutu wake hana uwezo, ila ni kwa sababu alipungukiwa maarifa ya kutosha ktk eneo husika.

11.Mwandishi ameonesha kuwa nguvu kubwa ktk aina ya maneno unayozungumza ina sababisho na matokeo ktk maisha yako. mfano huwezi kuwa tajiri kwa kunena umaskini na huwezi kuwa maskini kwa kunena utajiri, Bali kila mtu apandacho ndicho avunacho huwezi kupanda dhambi harafu ukavuna mbingu.

12.Mwandishi ameonesha kuwa kila ambacho tunakiona (matokeo ya nje) ndivyo tulivyo ndani kwa maana nyingine hatuwezi kukuona unafanya vitu tofauti na jinsi ulivyo ndani yako, Namnukuu.”………Aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo”

13.Mwandishi ametufundisha lazima tufanye uchaguzi kwenye vyakula tunavyokula yaani tusibugie kila kilichopo mezani eti kwa sababu ni chakula. Lazima tuchague mawazo chanya ya kulisha akili zetu.

14,Mwandishi ameonyesha kwa uwazi kabisa kuwa kiwango chako cha elimu , cheo, aina ya taaluma(professional) siyo kigezo cha wewe kufanikiwa yako bali ni nguvu yako ya kuthubutu kwa kufanya vitu zaidi(beyong the scene) au out of the box

 1. Mwandish anaamimi kuwa mtu yeyote anayo nafasi ya kufanikiwa haijarishi background yake ila tu ikiwa atathubutu na kufanya maamuzi sahihi na kufanya kwa vitendo.

Jifunze kuwa bahili

Usinunue vitu vya gharama kubwa kwa ajiri ya kuwakomoa maadui zako,huo ni utoto na
ushamba
Badilika, ohoo!!!Usihonge mchepuko pesa nyingi wakati mkeo na watoto wanalala njaa,usihonge pesa nyingi Kwamademu zako na mahawala wakati WAZAZI WAKO kijijini wanakula maharage na
mchicha
Bila mafuta HIYO NI LAANA,shauri yako.
.
Usitoe msaada unaokuumiza kiasi cha kubaki na MANUN’GUNIKO MOYONI,usisaidie zaidi
ya
Uwezo wako,,jifunze hekima ya kuwa na kiasi,Mungu anapenda wale watoao kwa moyo waukunjufu,wala usitoe ili usifiwe,wala usitoe ili ubarikiwe,toa kwa kuwa umebarikiwa..
Usiingie kwenye MADENI MAZITO YA KUKUTOA ROHO kwa kutaka kujionesha kwamba
wewe ni mwema sana, hata YESU alikataa wasimuite MWEMA sasa wewe ni nani unayetaka
kuonekana mwema sana? Hakikisha wema wako unakuwa na kiasi na uendane na UWEZO
wako.

Kwa NINI UWEKEZE JATU NA KUNUNUA HISA ZA JATU PLC

KWA NINI UWEKEZE KWA KUNUNUA HISA ZA JATU?
Kuna sababu nyingi sana za kiuchumi na kijamii ambazo zinatosha kukushawishi wewe mtanzania
kuwekeza katika Kampuni hii kwa kununua hisa hasa katika kipindi hiki ambapo Kampuni inapeleka hisa
nyingine mpya sokoni. Baadhi ya sababu hizo ni kama ifuatavyo;

 1. Kushiriki katika miradi ya kilimo inayofanywa na Kampuni.
  Kampuni ya JATU inaendesha kilimo jumuishi kwa wanachama wake na moja ya vigezo ili kukidhi matakwa
  ya kulima na JATU ni pamoja na kuwa na hisa ambazo zinakadiriwa kuwa wastani wa hisa 500 au Zaidi.
 2. Gawio la faida itokanayo na usimamizi wa kilimo
  Pamoja na kwamba hisa zitakufanya uweze kulima na JATU, pia hisa hizi zitakuwezesha kupata gawio la
  faida kutokana na faida itokanayo na mapato ya wakulima ambao wanapolima huchangia 25% ya faida
  yote kwa kila ekari katika maendeleo ya Kampuni. Na hii 25% inapelekea faida ya Kampuni kuongezeka
  na hivyo kufanya gawio la faida kwa kila hisa mwisho wa mwaka kuwa kubwa na la uhakika.
 3. Kupata Uwakala wa Huduma za JATU
  Unapokuwa mmiliki wa hisa za JATU unakidhi vigezo vya kuwa wakala wa huduma za JATU PLC kama vile
  kuuza bidhaa za JATU ambazo kwa sasa zinapatikana nchi nzima baada ya kuzalishwa na viwanda vya
  JATU na kusambazwa kwenda kwa mawakala wetu. Ukiwa wakala wa bidhaa za JATU unauza na kupata
  gawio la faida kulingana na mauzo yako kila mwezi na ikumbukwe kwamba bidhaa hizi unazipata tuu kwa
  dhamana ya hizo hisa unazomiliki.
 4. Kuwa Mwanachama na Mnufaika wa JATU SACCOS LTD
  Ukiwa na hisa za JATU utaweza kushiriki katika huduma za JATU SACCOS Ltd ambapo utapata mikopo ya
  kilimo bila riba na mikopo ya maendeleo kwa mashart nafuu. JATU SACCOS pekee ndio taasisi inayotoa
  mikopo ya kilimo isiyo kuwa na riba Tanzania na ni suluhisho kwa changamoto zinazowakabili wakulima.
  Kupitia SACCOS hii, mkulima ataweka 1/3 ya gharama zote za kulima kama akiba na kupokea mkopo wa
  2/3 ya gharama zilizosalia. Mkulima atalima chini ya usimamizi wa JATU PLC na mara baada ya mavuno
  atarejesha mkopo huo bila riba yoyote.
 5. Kuwa Balozi wa JATU
  Ukiwa na hisa za JATU PLC unaweza kuwa balozi wa JATU kupitia JATU TALK na JATU Market.
  Kupitia JATU TALK utaweza kubuni wazo lolote la kibiashara linaloendana na shughuli za Kampuni, kisha
  Kampuni itakusaidia kukuunganisha na wawekezaji walio na mtaji na kukuwezesha kulifanya wazo lako
  kuwa biashara au Kampuni kubwa.
  Mfano mzuri ni wazo la mradi wa parachichi ambao unaendelea mkoa wa njombe chini ya usimamizi wa
  JATU PLC, ni wazo la wanachama wenye hisa ambao kwa kutoa tu wazo sasa ni wamiliki wa mradi huo
  kwa 25%. Fikiria mradi huu unategemewa kutoa faida ya bilioni 10 kwa mwaka, maana yake ni kwamba
  wenye wazo wanauwezo wa kutengeza bilioni 2.5 kwa mwaka huo. Hili ni wazo moja lakini unaweza kuwa
  na mawazo mengine mengi zaidi na ukatengeza faida lakini kumbuka ni lazima uwe na hisa za JATU PLC.
  Kuhusu ubalozi wa JATU Market, wahusika ni wakulima na wajasiliamali ambao wanafanya kazi zao za
  uzalishaji nje ya JATU, JATU inatoa fursa ya kuuza bidhaa binafsi kupitia JATU Market ambapo unaweza
  kuingia kwenye app ya JATU Market na kuweka bidhaa zako na kuuza kwa wanachama wa JATU.
  Watakaopewa kipaumbele ni wakulima na wazalishaji wa bidhaa za chakula. Zalisha kadri uwezavyo na
  lima kadri uwezavyo JATU itakupa soko la uhakika endapo unamiliki hisa za JATU.

SONGA MBELE

Leo nataka nikwambie kwamba unapaswa kuendelea KUSONGA MBELE hata kama unakutana na changamoto.

Tuseme kwamba upepo wa kisulisuli unatokea na wewe haupo mahali ambapo wanaochukuliwa na upepo wamekaa. Utakuacha tu!
imeandikwa kwamba kesheni maana hamjui siku wala saa. Vivyo hivyo, songambele bila kukata tamaa au kuacha maana haujui lini bahati yako itakuja.

Naupenda sana ule usemi wa Donald Trump anaposema kwamba, mtu huwa anakuwa na bahati pale ambapo fursa inakutana na maandalizi.

Ni wazi kwamba huwezi kuomba lifti wakati umelala chumbani kwako.
wewe unapaswa kuwa safarini ili akitokea mtu wa kukupa lifti basi ubahatike kufika mapema.
ukiwa safarini, unatembea akatokea mwenye baiskeli basi itakuwa nafasi yako kupata lifti.
akitokea mwenye bodaboda basi utakuwa na bahati zaidi.
akitokea mwenye gari basi hapo ndio kabisaa, umepata bonge la BAHATI.

Lakini hawa hawawezi kukuta chumbani kwako. Watakukukuta unatembea.
Nakuabaliana kwa asilimia zote na Martin Luther King Jr, aliywahi kusema hivi,
kwma huwezi kupaa, kimbia,
kama huwezi kukimbia tembea
kama huwezi kutembea basi tambaa. Kwa chochote unachofanya, endelea kusongambele

Mimi kwa sasa hivi sina la ziada.
Umekuwa nami,
JULIUS Michael
tuwasiliane kwa
0768242953

Kupata kitabu cha #KutokaSifuriMpakaKileleni kwa elfu 12 tu tuwasiliane. kwa 0768242953

Jinsi ya kuongeza ufanisi katika kazi yako

Wakati mwingine ili uweze kuwa bora kwenye kazi unayoifanya basi unatakiwa kuelewa vyema namna ambavyo utaweza kuwa bora katika kazi hiyo unayoifanya hatimaye upate matokeo yenye thamani mbele yako na watu wengine kwa ujumla.

Mara nyingi huwezi kusema unataka mafanikio katika kile ukifanyacho wakati huo huo umesahau kufanya mambo ya msingi yatayokusaidia kuwa hivyo. Kila wakati unatakiwa kuelewa ubora na uzuri wa kitu huwa unatengenezwa na muhusika wa kitu hicho.

Hivyo iwe umejiari au umejiriwa basi unatakiwa kuzingatika mambo ya muhimu ambayo nitakueleza katika makala haya namna ambavyo unaweza kuongeza ufanisi wa kiutendaji katika kazi zako kama ifuatavyo;

Ili uweze kuwa bora na kuongeza ufanisi katika kazi yako unayoifanya basi unatakiwa kujitambua mwenyewe. Katika suala la kujitambua wewe binafsi ni lazima ukae chini na kutafakari kuhusu mstakabali mzima wa maisha yako.

Unapofanya tafakari kuhusu wewe, unatakiwa kujua wewe ni nani? unataka kufanya nini na kwa muda gani? Na unataka kufanikiwa kwenye eneo gani hasa?. Vile vile ni lazima uelewe kusudio la kuumbwa kwako.

Kila mwanadamu ameubwa kwa kusudio lake hapa dunia hivyo ni lazima mtu huyo aweze kutumikia hilo kusudio lake, kama ni kipaji basi unatakiwa kikutumia vyema hivho kipaji, kama ni biashara basi unatakiwa kuifanya vyema.

Kila wakati unatakiwa kujihoji maswali muhimu ambayo yatakusaidia sana kuweza kujitambua wewe mwenyewe, kwa kila swali ambalo utakuwa unajihoji unatakiwa kutafuta majibu sahihi ya maswali hayo.

Unatakiwa kufanya hivyo kwa sababu watu wengi tumekuwa tukiishi maisha ya ukawaida sana au kwa maneno mengine maisha ya kimazoea na ndiyo maana hata matokeo ya vitu tunavyovifanya vimekuwa vikileta matakoe kawaida pia.

Hivyo ili kuepukana kupata matokeo ya kawaida kwenye vitu tunavyofanya tunakiwa kuwekeza muda mwingi katika kujitambua sisi mwenyewe kwa kuangalia malengo yetu na kazi ujumla.

Vile vile ili uweze kupata matokeo chanya kwenye kazi unayoifanya basi uanatakiwa kufanya kitu cha tofauti. Katika dunia hii karibia asilimia 50 ya vitu vinavyofanywa na mwanadamu ni kwamba vitu hivyo vinafanana, Hivyo ili kupata matokeo tofauti na watu wengine basi uanatakiwa kuongeza thamani zaidi katika kitu hicho ili kujitofautisha na watu wengine.

Kwa mfano kama unauzaa mchele fahamu kila mtu naye anafanya biashara hiyo ya kuuza mchele, swali la kujiuliza ni je unajitofautishaje na watu wengine wanaofanya biashara kama yako?

Kila wakati ili uweze kuongezea thamani katika kazi basi unatakiwa kuelewa namna ambayo utajitofautisha wewe na watu wengine wanaofanya kitu kinachofanana na wewe.

Lakini mbinu nyingine ambayo itakufanya uongeze ufanisi wa kiutendaji katika kazi unayoifanya ni kutafuta muda wa kufanya kitu kimoja kwa umakini kazi unayoifanya. Kwa mfano kwa siku tunayo masaa 24 hivyo inatakiwa masaa mawili tu ya kufanya kitu cha maana.

Masaa haya mawili kwa kitaalum huitwa na masaa ya dhahabu, yaani muhusika anatakiwa kuweka nguvu nyingi za umakini katika kufanya kazi katika masaa hayo. Pia katika masaa hayo mawili unatakiwa kuelewa kwamba mawazo yako yanatakiwa kutulia katika kufikiri na kufanya kazi kwa umakini wa hali ya juu sana ili kupata matokeo chanya katika kazi hiyo unayoifanya.

Ukiyazingatia hayo mambo muhimu niliyokujuza siku ya leo katika makala haya basi maisha yako yatabadilika kwa kiasi kikubwa sana.

Elimu ya msingi ya pesa

UKOSEFU WA ELIMU YA MSINGI YA FEDHA HUTUPELEKEA KUWA MASKINI . JIFUNZE HAYA USIYOYAJUA KUHUSU ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.

( 1 ).FEDHA SIYO MAKARATASI.
Watu wengi wamekuwa wanafikiria fedha ni yale makaratasi au sarafu ambazo tunazishika. Na hapa ndipo wengi wanapokwama, kwa sababu wanakosa ule msingi muhimu kuhusu fedha. Kwa kukosa msingi muhimu kuhusu fedha, watu wanashindwa kuzipata kwa wingi na hata kuzitumia vizuri.
Fedha ni wazo ambalo lina thamani. Fedha ni matokeo ya mtu kuwa na wazo ambalo linaongeza thamani kwa wengine. Bila ya thamani hakuna fedha. Hivyo kama unataka fedha zaidi, lazima ujue thamani gani unatoa kwa wengine.

( 2 ).KIPATO KIMOJA NI UTUMWA.
Kuwa na chanzo kimoja cha kipato pekee ni utumwa. Huwezi kuondoka kwenye umasikini kama unategemea kipato chako kitoke sehemu moja pekee. Kama umeajiriwa pekee, hata kama unalipwa kiasi kikubwa cha fedha, bado unabaki kwenye umasikini. Kama unafanya biashara na unategemea wateja wachache nayo pia inakuweka kwenye umasikini.
Utaondoka kwenye umasikini kwa kuwa na vyanzo vingi vya kipato. Bahari huwa haikauki kwa sababu mito mingi inaishia kwenye bahari. Hiyo kama unataka usikaukiwe na fedha, kuwa na vyanzo vingi vya kipato.

(3) MATUMIZI NI BOMU.
Watu wengi wamekuwa wanaanza maisha na kipato kidogo, na yanaenda. Kipato kinaongezeka na matumizi yanaongezeka, kila kipato kinapoongezeka na matumizi pia yanaongezeka. Matumizi ni bomu kama hayatadhibitiwa. Matumizi yana tabia ya kuongezeka pale tu kipato kinapoongezeka.
Huwezi kuondoka kwenye umasikini kama huwezi kuyadhibiti matumizi yako. Haijalishi unatengeneza kipato kikubwa kiasi gani, matumizi ni bomu, usipolitegua litakulipua.

( 4 ).MADENI NI UTUMWA.
Umesikia hapo, na najua huenda kimoyomoyo unakataa, unajiambia siyo kweli, kwa sababu huenda umeshalishwa sumu kwamba bila madeni maisha hayawezi kwenda. Unajua nini, wale wanaonufaika na madeni ndiyo wanasambaza propaganda za aina hiyo. Madeni ni utumwa, na huwezi kuondoka kwenye umasikini kama huwezi kuondokana na madeni.
Kuna madeni mazuri na mabaya, na masikini wote huwa wapo kwenye madeni mabaya. Madeni mabaya ndiyo yanawafanya watu kuwa watumwa, wanajikuta wanafanya kazi sana kulipa madeni, halafu wanakopa tena. Kwa hiyo maisha yao yote yanakuwa mzunguko wa kopa, lipa, kopa tena.

( 5 ).BIASHARA NI MKOMBOZI.
Zile zama za nenda shule, soma kwa bidii, faulu na utapata kazi nzuri na inayolipa zimeshapitwa na wakati. Kila mtu anaona wingi wa watu wenye sifa za kuajiriwa, lakini hakuna nafasi za ajira. Na hata walioajiriwa, mazingira ya kazi na hata kipato wanachoingiza hakiridhishi.
Kwa zama tunazoishi sasa, mkombozi pekee, kitu pekee kitakachokuwezesha kuwa na maisha mazuri ni kuwa na biashara yako. Hivyo ni muhimu sana uwe na biashara kama unataka kutoka kwenye umasikini.

( 6 ). UWEKEZAJI NI KIJAKAZI WAKO.
Inapokuja kwenye fedha, kuna mambo mawili, kuna kuifanyia kazi fedha, pale ambapo inabidi ufanye kazi ndiyo fedha iingie. Halafu kuna fedha kukufanyia kazi wewe, ambapo fedha inaingia hata kama hufanyi kazi moja kwa moja.
Ili kuondoka kwenye umasikini na kufikia uhuru wa kifedha, ni lazima fedha ziwe zinakufanyia kazi wewe. Na hapa ndipo unapohitaji kuwa na uwekezaji, ambao unafanya kazi ya kuuzalishia fedha, hata kama wewe umelala.
( 7 ). KODI NI UWEKEZAJI.
Kodi ni gharama unayolipa kwa kuishi kwenye jamii iliyostaarabika. Ni kodi tunazolipa ndiyo zinazoleta huduma mbalimbali tunazozitegemea kwenye jamii. Huduma za afya, huduma za elimu, ulinzi na usalama, miundombinu kama barabara na mengineyo ni matokeo ya kodi tunazolipa.
Hivyo kodi ni uwekezaji ambao kila mmoja wetu anapaswa kuufanya ili tuwe na jamii bora. Tunapaswa kuondokana na dhana potofu kwamba kodi ni kitu kibaya. Kwa sababu hebu pata picha, umekazana kutafuta fedha na ukawa tajiri, halafu unaishi sehemu isiyo salama, je utaweza kufurahia utajiri wako?
( 8 ).BIMA NI MKOMBOZI.
Kuna hatari mbalimbali ambazo zinatuzunguka kwenye maisha, na kadiri unavyopiga hatua kifedha, ndivyo hatari zinakuwa kubwa zaidi. Hili limekuwa linazua hofu kwa wengi na wakati mwingine kuwazuia hata kufanikiwa.
Ili kuondokana na hatari zinazokuzunguka na kukuzuia kuanguka pale unapokutana na changamoto kubwa, unapaswa kuwa na bima. Kwa bima unachangia kiasi kidogo cha fedha, lakini unapopata tatizo, unalipwa kiasi kamili cha fedha au mali ulizopoteza.

( 9 ). WATOTO WAKO HAWAHITAJI FEDHA ZAKO.
Wazazi wengi wamekuwa wanakazana kutafuta fedha na mali kwa wingi, ili kuwaachia watoto wao urithi na wasiwe na maisha magumu. Lakini wote tumekuwa tunaona nini kinatokea baada ya wazazi hao kufariki, utajiri na mali zote zinapotea, kwa kutumiwa vibaya na watoto walioachwa.
Watoto wako hawahitaji sana fedha wala mali zako, bali kikubwa wanachohitaji ni msingi muhimu wa kufuata na kusimamia inapokuja kwenye swala la fedha. Kuliko uwape watoto fedha bila ya misingi, ni bora uwape misingi bila ya fedha. Kwa sababu misingi itawawezesha kupata fedha zaidi wakati fedha pekee bila misingi zitapotea.

( 10 ). KUTOA NI UWEKEZAJI.
Mmoja wa watu matajiri sana kuwahi kuwepo hapa duniani, John D. Rockefelar amewahi kunukuliwa akisema unatumia nusu ya kwanza ya maisha yako kukusanya fedha, halafu nusu ya pili unaitumia kuzigawa fedha hizo kwenda kwa wengine.
Moja ya vitu vinavyowafanya matajiri kuendelea kuwa matajiri ni utoaji. Matajiri wengi wamekuwa watoaji wa misaada mbalimbali ya kijamii na hilo limekuwa linawasukuma kufanikiwa zaidi kifedha. Hivyo kutoa ni uwekezaji ambao unamlipa sana mtu baadaye.

Create your website with WordPress.com
Get started